MAMBO MATANO YATAKAYOKUFANYA UANZE KUWEKA AKIBA

August 26, 2019
“Fursa za kutajirika zimejificha. Zinapojitokeza huchukuliwa kwanza na watu wenye tabia ya kuweka akiba. Hivyo kuna kila sababu ya kuweka akiba”

Wanaochangamkia fursa na kustawisha maisha yao ni wale wote wenye tabia hii muhimu ya kuweka akiiba.

 1;TENGA FUNGU LA KUMI KWENYE KIPATO CHAKO;
Hakikisha kila fedha unayoipata kama kipato kwako unatenga fungu la kumi kama akiba. Tenga fungu la kumi kama akiba kwa kila kiasi unachokipata hata kama ni kidogo kiasi gani. Kama ni mshahara, kila mwenzi weka asilimia kumi pembeni kama akiba. Ukifanya hivi utajikuta taratibu unajenga tabia ya kuweka akiba. Kuna wakati utafika utaweka akiba zaidi ya asilimia 10 kutokana na tabia ya kuweka akiba kujengeka ndani yako.


2; EPUKANA NA MATUMIZI YASIYO NA ULAZIMA..
Epuka kabisa kufanya matumizi yasio na ulazima. Kama ndiyo unaanza kujenga tabia ya kuweka akiba.  Kabla ya kufanya matumizi yoyote jiulize kwanza maswalia haya; kwa nini nifanye matumizi haya; nini faida ninayopata kwa matumizi haya, na je hii pesa ya haya matumizi haiwezi kutumika kwenye mambo mengine ya muhimu zaidi? Tabia hiyo ya kujiuliza maswali kabla ya kufanya matumizi yoyote itakusaidia kutathimini na kujua nini cha muhimu na nini si cha muhimu.

3; ANZA KUWEKA AKIBA KIASI KIDOGO;
Kwa sababu watu wengi hawaweki akiba kwa kisingizio cha kwamba kipato ni kidogo, basi anza kuweka akiba  na kiasi kidogo kulingana na kipato unachokipata. Kadri utakavyoweka akiba kwa kiasi kidogo ndivyo utapata nguvu ya kuweka akiba kiasi kikubwa zaidi na zaidi siku zinavyokwenda. Usitake kuweka akiba kiasi kikubwa kama unaanza kwa sababu utashindwa mapema. Usikatishe matumizi yako ya zamani uliyokuwa umeyazoea ghafla. Kukata ghafla ni kuilazimisha akili ikukubalie kuanza tabia mpya bila ya kuizoesha tabia mpya, kufanya hivyo ni hatari. Usifanye hivyo wewe nenda mdogo mdogo. Utapata nguvu zaidi ya kuweka akiba kadri siku zinavyosoge, na itakuja kuwa ni utamaduni wako wa kawaida.

“aliyemwaminifu kwa kidogo ataongezewa bali yeye azuiaye (asiyewekeza) hata kidogo alichonacho(anachosema hakitoshi kuweka akiba wala kuweka akiba) atanyanga’anywa”

4;TENGENEZA MPANGO WA MATUMIZI.
Ili uweke akiba jambo la muhimu sana kwako ni kutengeneza mpango wa matumizi kabla ya kufanya matumizi yoyote ya fedha . Hapa namaanisha lazima ukae chini uchukue kalamu na karatasi. Andika kiasi ulichonacho au unachotegemea kukipata baada ya hapo anza kuorodhesha matumizi muhimu utakayo yafanya na achana kabisa na matumizi yasiyo na umuhimu. Ukishafanya hivyo tenga fedha ya kuweka akiba na kwa ushauri wangu anza na asilimia kumi ya pato lako. Kumbuka nidhamu kwenye hili ni suala la muhimu sana, hakikisha hufanyi matumizi yoyote nje ya mipango uliyojiwekea.


4; JENGA MTIZAMO WA KUWEKA AKIBA KWENYE KILA FEDHA UNAYOIPATA.  Hapa namaanisha kwamba kila kitu kinaanzia ndani mwetu. Huwezi kuanza kuweka akiba kama huna mtizamo huo. Anza kusema na akili yako na kujiambia ni lazima niweke akiba, fanya hili zoezi mara kwa mara pia anza kusoma vitabu na makala zinazohusu masuala ya fedha. Utaanza kuona mabadiliko katika mtizamo wako. Usikubali taarifa za watu kuwa kipato kidogo hakiwezi weka akiba, puuza na waone kama watu wasiojali hatma zao.

5;BADILISHA MAZINGIRA.
. Kwa asilimia kubwa mazingira yanachangia kutengeneza tabia na mtizamo ulionao. Hapa nazungumzia marafiki na watu wanaokuzunguka. Watu wanaokuzunguka wana athari kubwa sana katika tabia zako. Kama ulikuwa unapenda kampani za kula bata acha na anza kutumia huo muda wakula bata kufanya mambo mengine chanya.

No comments:

Powered by Blogger.