AKIBA NI NINI?

September 03, 2019
AKIBA NI NINI?/ WAKATI WA KUWEKA AKIBA.


AKIBA: SEHEMU YA MIPANGO YA MTU KATIKA KUKUZA UCHUMI WAKE KWA SIKU ZIJAZO AU MATUMIZI YAKE YA WAKATI UJAO.

Uchumi wa mtu hukua kidogo kidogo kupitia kile anachopata na kisha kuweka moja ya sehemu yake kama akiba. Uchumi wa siku za usoni wa mtu unategemea akiba anayoweka leo kidogo kidogo katika kile anachopata kila siku, au kila wiki, au kila mwezi. Kwa sababu hiyo, katika akiba hiyo kuna ongezeko la kiuchumi hutokea ambalo litakuwa na manufaa katika siku za usoni.
 We

AKIBA NI NINI?

Akiba ni kitu kilichotengwa na kuhifadhiwa vizuri na katika hali ya usalama kwa ajili ya matumizi muhimu ya baadaye.

Akiba ni maandalizi ya kujibu tatizo la kesho au kukizi uhitaji wa kesho. Mara nyingi akiba hujengwa kwa ajili ya uhitaji wa kesho ambao mtu kauona leo kupitia jicho la mipango yake katika kutimiza malengo yake au maono yake.

Akiba ni sehemu ndogo ya kile kinachopatikana leo inayotengwa na kuhifadhi pembeni pasipo kuitumia kwa sababu ni maalumu kwa ajili ya kesho.

Watu wanao weka akiba ni wale wanaoiona kesho yao. Kwa sababu akiba sio kwa ajili ya matumizi ya sasa isipokuwa ya kesho, ni wale tu wenye kuipanga kesho yao ndio wanapata nguvu ya kuweka akiba kwa ajili ya kesho.

Akiba si kinachosalia katika kile unachokipata, ni sehemu ya mpango wa mgawanyo wa kile unachokipata. Kama huna mpango na mgawanyo unaoeleweka daima huwezi kuweka akiba na badala yake utatumia chote unachokipata.

Ni ngumu sana kuweka akiba kama huna mpango, na huwezi kuona umuhimu wa akiba kama huna malengo. Mpango unakusaidia wewe kufikia malengo yako, kama huna malengo huwezi kuwa na mpango au mipango na kama huna mpango au mipango huwezi kuweka akiba kwa sababu "akiba ni mpango wenye lengo la kukunufaisha hapo baadaye katika kutatua changamoto zitakazojitokeza na hasa kwa ghafula ili kukuzuia wewe kufikia malengo yako

"

Akiba inakwenda au inawekwa kulingana na kipato chako. Katika kila unachokipata jifunze kuweka akiba. Mpaka akiba imekuwa ni sehemu ya kila unachopata ndipo unaweza kuweka akiba na kunufaika nayo.

Kila mmoja ili mradi ana akili timamu analazimika kuweka akiba, kama si kwa ajili yake basi ni kwa ajili ya watoto wake. Nirudie tena, "akiba ni mpango unaolenga kutimiza malengo fulani ya muhimu na ya lazima ambayo si rahisi kuyakwepa katika siku za usoni."

Wewe ni kijana au ni binti hujaoa au hujaolewa lakini unatarajia kuoa au kuolewa na hatimaye uwe na watoto wako mwenyewe, basi weka akiba kuanzia sasa kwa ajili ya watoto wako, weka akiba kwa ajili ya ujenzi wa nyumba yako, weka akiba kwa ajili ya harusi yako na kadhalika. Na kwa sababu hujui ni baa au janga gani litatokea baadaye akiba ni swala la muhimu sana.

Moja ya faida kubwa ya akiba ni inapunguza gharama kama sio kumaliza kabisa gharama za kutimiza malengo yako.

AKIBA INAWEKWA WAKATI GANI?

Akiba huwekwa wakati vitu (ama fedha) inapatikana iwe ni kila siku, au kila wiki au kila mwezi au katika kila majira. Akiba huwekwa wakati wa upatikanaji wa vitu au fedha, wakati vipo na vinapatikana (wakati wa mavuno) ndio wakati wa kuweka akiba. Kwa lugha rahisi ni kwamba, kila unapopata ndipo unapoweka akiba, wakati unapopata ndio wakati unapoweka akiba yako.

Masikini wa kesho ni wale wasioweka akiba leo ya utajiri wao wa sasa. Tajiri wa sasa au leo asiyeweka akiba leo kwa ajili ya kesho anajiandaa kuwa masikini wa kesho na muhitaji asiyeweza kutimiliza uhitaji wake kabisa, na kwa sababu hiyo atakuwa omba omba.

AKIBA NI MSINGI MZURI KWA WAKATI UJAO.
HADI HAPO NAJUA  UTAKUA UMEJIFUNZA NINI MAANA YA AKIBA NA NI WAKATI GANI SAHIHI WA KUWEKA AKIBA. 
KAMA UNAHITAJI CASHBOX/VIBUBU VYA KISASA KWAAJILI YA KUHIFADHIA PESA TUPIGIE. #0679858408

No comments:

Powered by Blogger.