FAIDA TANO ZA KUWEKA AKIBA

August 17, 2019
SIKU ZOTE VITU VIKUBWA  VINATOKANA NA VITU VIDOGO. JIFUNZE KUDUNDULIZA KIDOGO KIDOGO.

*FAIDA TANO ZA KUWEKA AKIBA*

1: KUJIANDAA KWA DHARULA.

Watu wengi huingia kwenye madeni au kupata uhitaji mkubwa wa pesa mara wapatwapo na dharura. Hivyo kwa kuweka akiba utapata faida ya kukuepushia mahangaiko wakati wa dharura kama vile maradhi, msiba, majanga, n.k.


2: KUWEZA KUFANYA MANUNUZI AU MIRADI YA GHARAMA KUBWA.

Kuna manunuzi au miradi ambayo inahitaji pesa nyingi ili kuitekeleza. Maswala kama vile ujenzi wa nyumba, ununuzi wa kiwanja, kununua gari, n.k. ni baadhi ya mambo yanayohitaji fedha nyingi.

Hivyo, kwa kuwa na akiba utaweza kutekeleza mambo haya kwa urahisi zaidi kuliko ungeyafanya bila akiba.

3: KUWEZA KUMUDU WANAOKUTEGEMEA .

Ikiwa kuna watu wanaokutegemea kama vile wazazi, ndugu au watoto; ni vyema kuweka akiba ili uweze kuwa na fedha ya kukidhi mahitaji yao mara wapatwapo na uhitaji.

Kutokuweka akiba kutakufanya uhangaike huku na huko ukitafuta fedha za kukidhi mahitaji ya wategemezi wako kama vile chakula, matibabu au hata ada za shule.

4:UTULIVU WA AKILI.

Unapokuwa huna akiba yoyote huwezi kuwa na utulivu wa akili. Kila wakati unahofu na wasiwasi juu ya maisha yako, unajiuliza likitokea tatizo itakuaje? Au hitaji fulani linalokuja hivi karibuni litakuwaje? n.k.

Unapokuwa na fungu fulani la akiba huna haja ya kuwa na wasiwasi kwani unajua hata ukikosa fedha akiba yako itakusaidia.

5: HUKUWEZESHA KUWAI FURSA.

Ni mara ngapi umekuwa ukisema au ukisikia kauli kama vile “Ningekuwa na pesa ningenunua hiki kitu”, “Ningekuwa na pesa ningejiunga kwenye hii huduma”, “Ningekuwa na pesa ningejiunga na huu mradi”, n.k.

Hili linadhihirisha kuwa watu hukosa fursa mbalimbali kutokana na kukosa akiba ya fedha. Unapokuwa na akiba ya fedha ni rahisi kuwahi fursa mpya au bidhaa zenye manufaa mara zinapopatikana.

Vibubu hivi vinauzwa

Inch 6 tshs 30,000 vinatumia funguo na code, pia waweza kusevia had tshs 2million.

Inch 8 tshs 40,000 kinatumia funguo na code waweza kusave had tshs 4million.

Inch 10 tshs 50,000 kinatumia funguo tu .kina uwezo was kusevia hadi tshs 6 million

Inch 12 tshs 60,000 kinatumia tu funguo. Kina uwezo was kusevia hadi tshs 8 million.

KAMA UNAPATA CHANGAMOTO YOYOTE JINSI YA KUWEKA AKIBA  .
TUPIGIE KWA USHAURI ZAIDI.#0679858408
#0679858408
#0679858408

No comments:

Powered by Blogger.